Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Historia imeandikwa Mwanariadha nyota wa Tanzania, Alphonce Felix Simbu, ameingia kwenye vitabu vya kumbukumbu baada ya kutwaa Medali ya dhahabu ya kwanza ya dunia kwa Tanzania katika mbio za marathoni za mabingwa wa dunia, zilizofanyika Septemba 15, 2025 jijini Tokyo.
Simbu mwenye umri wa miaka 33 alimaliza mbio kwa muda wa 2:09:48, akimshinda Mjerumani Amanal Petros kwa tofauti ndogo zaidi katika historia ya mashindano haya sekunde 0.03 pekee na kushinda Medali hiyo.
Baada ya Kutwaa Medali hiyo Simbu alisimulia jinsi safari yake ilivyo kuwa mpaka kufikia mafanikio aliyoyapata hapo Jana.
"Nimeandika historia leo Medali hii ni ya kwanza kwa Tanzania, Nakumbuka mwaka 2017 nilichukua shaba London, kisha nikajaribu mara nyingi bila mafanikio Safari hii niliahidi sitakata tamaa, naona matunda ya uvumilivu," alisema Simbu kwa furaha baada ya ushindi wake.
Kwenye hatua za mwisho, mashabiki walilipuka kwa shangwe walipoona pambano la ana kwa ana kati ya Simbu na Petros Simbu alionyesha kasi ya ajabu kwenye mita 10 za mwisho na kuvuka mstari wa mwisho akiongoza, jambo lililomfanya Petros kubaki na masikitiki.
Kwa ushindi huu, Simbu anaongeza dhahabu kwenye kumbukumbu yake baada ya shaba aliyopata London 2017, na pia kufuatia nafasi ya pili kwenye Boston Marathon 2025 Tanzania sasa imetambulishwa upya katika ramani ya riadha duniani, na jina la Simbu limebaki kama alama ya uthubutu, uvumilivu na fahari ya taifa.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment