Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Mkurugenzi wa sheria ,habari na masoko wa TFF Boniface Wambura ameelezea mwenendo mzima kuusu mustakabali wa tuzo kwa wachezaji katika msimu uliomalizika ambapo ukimya ulitawala bila kujua nini kinacho endelea na amesema kuwa tuzo zipo.
Wambura ameyasema hayo leo wakati akifanyiwa mahojiano na kituo kimoja cha redio hapa nchini, amesema kuwa tarehe za tuzo zitatangazwa sikuchache mbele ambapo itakuwa ndani ya mwezii wa tisa kwasababu suala hilo ni lakikanuni na hawawezi kuacha kufanya .
Aidha ameongeza kuwa kuna uwezekano wa tuzo kutolewa wakati ambao ligi itakuwa imeanza lakini kilicho pelekea hatua hiyo ni kutokana na maboresho wanayo ya fanya ambapo maboresho hayo yanaweza kupelekea ucheleweshwaji wa zoezi hilo ,muda utakapofika watatoa taarifa ni lini hasa tuzo zitatolewa na ni maboresho yapi waliyo ya fanya.
Pia amegusia kilicho pelekea uchelewashaji huo ni kutokana na kubanana kwa ratiba ikiwemo kuwepo na mashindano ya CHAN ambayo yalifanyika nchini huku Tanzania akiwa mshiriki mmoja wapo.
Wadau wa soka nchini waliingiwa na sintofahamu baada ya ukimya huo wa muda mrefu huku ligi ikiwa imekaribia kuanza , sasa ni muda wa kutulia na kusubiri mamlaka zinazo ongoza mpira nchini kuja kutaja tarehe ya tuzo kama alivyo ahidi mkurugenzi wa ,habari na masoko wa TFF.
0767915473,
Lugembetimothy01@gmail.com
Post a Comment