ENG.HERSI: HATUMUUZI MZIZE KWA GHARAMA YOYOTE

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Raisi wa klabu ya Yanga muhandisi Hersi Saidi ameweka wazi dhamira yao ya kuto kumuuza mshambuliaji nyota wa klabu hiyo Clement Mzize licha ya ofa lukuki zinazotoka nje ya nchi kuhitaji huduma ya mchezaji huyo.

 ameyasema hayo kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa klabu hiyo huku malengo makuu yakiwa ni kujadili mustakabali wa klabu hiyo kuelekea msimu ujao pamoja na kutaja mapato na matumizi ya msimu uliomalizika na kuelekea msimu ujao.

Clement Mzize tunamuhitaji kwa msimu huu hatuwezi kumuuza kwa kiasi chochote atabaki msimu huu na ataitumikia klabu , tunafanya hivyo kwasababu tunataka mafanikio hivyo hatuwezi kuruhusu silaha yetu ikatoka kirahisi.

Aidha amesema kuwa klabu hiyo ilipokea ofa kubwa zaidi ya kiasi cha dola laki mbili cha kumuitaji mcheaji huyo lakini klabu imeamua kumbakisha kutokana na uitaji wa mchezaji huyo kwenye kikosi chao kuelekea msimu mpya wa mashindano ambao wamepanga kufanya vizuri zaidi kwenye mashindano ya  ndani pamoja na ligi ya mabingwa barani Afrika, ingawaje wanaweza kufikiria kuuza mwishoni mwa msimu ujao.


Ofa ya mwisho ya Mzize ilikuja ya dola laki mbili lakini tukasema hauzwi kwa bei yoyote. Tunahitaji mafanikio hatuwezi kuuza silaha zetu muhimu. Msimu huu ukiisha tunaweza kufikiria kufanya biashara.

Wadau wa soka nchini wameipongeza klabu ya Yanga kwa kuendelea kuwabakisha wachezaji wake muhimu wa kikosi cha kwanza kama Clement Mzize na wengine kwani moja ya kitu muhimu kwenye klabu kama inahitaji kufanya vizuri ni kuwabakisha wachezaji wake muhimu na kufanya maingizo ya wachezaji bora ili kuendelea kufanya vizuri Zaidi, ingawaje baadhi ya wadau wengine hawajafurahishwa na kitendo cha klabu hiyo kutomfungulia milango mshambuliaji huyo akapate malisho bora zaidi.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.

 

0/Post a Comment/Comments