BALAA LA MAYELE LAVUKA MIPAKA, AIPA PYRAMIDS USHINDI KWA HAT-TRICK

 Timothy Lugembe ,

Mwanakwetusports.

Mshambuliaji hatari wa timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Fiston Kalala Mayele , ameonyesha ubora wake wa hali ya juu kwa kufunga magoli matatu (Hat-trick) na kuipeleka klabu yake ya Pyramids FC ya Misri hatua inayofuata katika mashindano ya FIFA International Cup 2024/25.

Katika mchezo huo uliojawa ushindani uliochezwa dhidi ya Al Ahli ya Saudi Arabia klabu kubwa yenye nyota wakongwe kama Riyad Mahrez, Ivan Tone na Edouard Mendy , Mayele alidhihirisha ubora wake wa kimataifa kwa kuamua matokeo kwa miguu yake.kwa kuweka kimiani mabao matatu na kuhitimisha safari ya Al Hali katika mashindano hayo.

Hat-trick hiyo si tu ilimfanya Mayele kuwa shujaa wa mchezo, bali pia imemuweka katika orodha ya washambuliaji bora zaidi barani Afrika wanaoendelea kutikisa soka la kimataifa.

Kwa mara nyingine tena, Mayele amethibitisha kuwa ni moto wa kuotea mbali na anabaki kuwa chachu ya mafanikio ya Pyramids FC, akiwasha moto na kuibua matumaini makubwa ya kutwaa taji la kimataifa.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments