AUCHO KUREJEA YANGA JANUARY

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyanzo vya michezo nchini Uganda, kiungo mkabaji wa kimataifa wa Uganda, Khalid Aucho, anatarajiwa kurejea klabuni Young Africans SC (Yanga) katika dirisha dogo la usajili mwezi Januari.

Aucho, ambaye aliwahi kuwa mhimili mkubwa katika safu ya kiungo ya Yanga, anajulikana kama mchezaji mwenye nguvu, anayependa kupora mipira, kupunguza kasi ya wapinzani na kusambaza pasi fupi kwa ustadi , Uwepo wake mara nyingi uliwapa Yanga uwiano wa ulinzi na mashambulizi, jambo lililowasaidia kutawala mechi nyingi za Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kwa sasa, Aucho anachezea klabu ya Singida black stars ambapo anaonyesha kiwango bora katika michezo michache aliyo cheza na bado ni nguzo muhimu katika timu ya taifa ya Uganda (The Cranes), akiwa na uzoefu mkubwa wa kimataifa unaowafanya makocha kumwamini katika mechi kubwa.

Kama atarejea Jangwani kunatarajiwa kuongeza ubora wa safu ya kiungo ya Yanga, hususan katika mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika na Ligi Kuu Bara, kwani mashabiki wengi bado wanamkumbuka kwa namna alivyokuwa mhimili wa kutuliza mchezo na kusukuma timu mbele.

Ieleweke kwamba Kuna uwezekano wa mchezaji huyo kurejea Yanga ila sio rasmi na hiyo nikwamujibu wa vyanzo kutokea nchini kwao Uganda.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments