Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports
Kiungo mkabaji wa Yanga SC, Aziz Andambwile, ameendelea kuonyesha kiwango cha juu katika michezo miwili muhimu iliyochezwa na klabu hiyo hivi karibuni, Andambwile aliwapa tafakari mashabiki wake kwa utendaji wa hali ya juu kwenye Ngao ya Jamii dhidi ya Simba SC na kwenye mchezo wa Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Wiliete SC ya Angola.
Ngao ya Jamii: Yanga SC 1–0 Simba SC
Mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Andambile alicheza kama kiungo mkabaji, akichangia sana kuzuia mashambulizi ya Simba na kuanzisha mashambulizi ya Yanga , kabla ya Yanga kuanza kucheza mashabiki walitafakari zaidi kuhusu pengo la Khalid Aucho alietimkia Singida black stars lakini mawazo hayo yalizimwa na ubora wa Andambwile kwenye mchezo huo ,Ingawa hakufunga bao, alionyesha ustadi wa hali ya juu katika mpangilio wa kiungo, akichangia ushindi wa 1-0 kwa Yanga, bao pekee likifungwa na Pacome Zouzoua dakika ya 54.
Klabu Bingwa Afrika: Wiliete SC 0-3 Yanga Sc
Katika mchezo wa kwanza wa mzunguko wa awali wa CAF Champions League, Andambwile ameibua mjadala kwa mashabiki wa Yanga na wadau wa soka alipofunga bao la mbali la kuvutia dakika ya 32, akipiga shuti lililokuwa ngumu kwa kipa wa Wiliete bao hilo lilifungua mlango kwa ushindi wa 3-0, huku mabao mengine yakifungwa na Edmund John (72') na Prince Dube (83) katika mchezo huo amezidi kushika Imani za mashabiki na wanasoka nchini kuwa anastahili kuwa kwenye nafasi aliyopo na kiwango chake kinazidi kumfanya kocha amuamini zaidi.
Kwa mashabiki wa Yanga SC, Andambwile anazidi kuthibitisha kuwa ni mmoja wa wachezaji wa muhimu wa timu, huku akionyesha ustadi wa kipekee wa kiungo mkabaji na uwezo wa kushambulia.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment