AL AHLY WATIMUA KOCHA , MISHAHARA NAYO YAPUNGUZWA

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Klabu ya soka ya Al Ahly imejikuta katika mtikisiko mkubwa baada ya uongozi wake kutangaza rasmi kupunguza mishahara ya wachezaji kwa asilimia 25 na kumtimua kocha wake.

Hatua hiyo imechukuliwa kufuatia msururu wa matokeo mabovu ambapo timu hiyo imeshinda mchezo mmoja pekee kati ya michezo walizocheza hivi karibuni.

Katika msimamo wa ligi, Al Ahly inashikilia nafasi ya 13 ikiwa na alama tano , timu hiyo imeshinda mchezo mmoja, kutoa sare michezo miwili na kupoteza mchezo mmoja kati ya minne iliyopita, jambo lililozua sintofahamu miongoni mwa mashabiki na wanachama wake.

Kwa upande mwingine, wapinzani wao Al Masry wapo kileleni mwa ligi kwa alama 11 baada ya kucheza michezo mitano, timu hiyo imeibuka na ushindi mara tatu na kutoa sare michezo miwili, huku ikibaki pekee miongoni mwa timu ambazo bado hazijafungwa msimu huu.

Mbali na hatua ya kukatwa mishahara, klabu hiyo pia imemtimua rasmi kocha wake Jose Riveiro, Kocha huyo amewaaga wachezaji wake baada ya kushindwa kubadilisha mwenendo wa timu na kujikuta wakitaabika kwenye nafasi za chini katika msimamo wa ligi.

Hali hiyo imezidi kuongeza hofu kwa mashabiki wa Al Ahly ambao wamezoea kuona timu yao iking’ara, huku sasa wakibaki na maswali mengi kuhusu hatma ya kikosi hicho kinachojulikana kwa historia na mafanikio yake makubwa barani Afrika.

Swali ni je, hatua ya kuwapunguza mishahara wachezaji ni suluhu ya kupata matokeo Bora au ndio itaendelea kujenga vinyongo miongoni mwa wachezaji na kufanya vibaya zaidi? Majibu yatapatikana kwenye michezo inayofuata.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments