WYDAD NA SIMBA MAMBO SAFI KWA GOMEZ

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Klabu ya Simba SC imekamilisha uhamisho wa mshambuliaji Selemani Mwalimu (GOMEZ) kwa mkopo wa mwaka mmoja akitokea Wydad Athletic Club ya Morocco, ambapo katika mkopo huo Kuna chaguo la Simba kunmnunua mchezaji huyo kwa kwa Moja.

 Imeelezwa kuwa mchezaji huyo tayari amekubali masharti ya mkataba na atakuwa sehemu ya kikosi cha wekundu wa Msimbazi katika msimu mpya wa Ligi Kuu ya NBC na michuano ya kimataifa ya CAF.

Katika uhamisho huo timu ya Singida black stars hawapata gawio lolote mpaka pale Wydad watakapo muuza mchezaji huyo moja kwa Moja.

Mwalimu, ambaye ana uzoefu mkubwa barani Afrika kutokana na kucheza katika ligi yenye ushindani mkubwa ya Morocco pia kushiriki mashindano makubwa ya vilabu Duniani (FIFA CLUB WORLD CUP), anatarajiwa kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji ya Simba kwa kushirikiana na safu ya ushambuliaji akishirikiana na Mukwala na Jonathan Sowah.

Mashabiki wa Simba wamepokea kwa vizuri taarifa hizo, wakiamini kuwa ujio wa Mwalimu utasaidia klabu hiyo kufanikisha malengo yake ya kurejesha ubingwa wa ligi na kufanya vizuri zaidi kwenye michuano ya kimataifa.

Hii ni ishara nyingine kuwa Simba SC ipo tayari kufanya maboresho makubwa kuelekea msimu mpya, huku ikionekana wazi dhamira ya klabu hiyo ni kuhakikisha inabaki juu ya ushindani wa soka la Afrika.



0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments