Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN 2024) yanaendelea kushika kasi, huku mataifa wenyeji yakionyesha ubora wa hali ya juu katika hatua ya makundi, Hadi sasa, Tanzania, Kenya na Uganda wanaongoza makundi Yao huku wakisubiria michezo ya mwisho kujihakikishia nafasi hiyo.
Katika kundi B Kikosi cha Taifa Stars kimetumia vyema faida ya kucheza nyumbani, kikishinda mechi zote tatu za Kundi B na kujikusanyia alama 9 , huku ukiwa umebaki mchezo mmoja pekee kujihakikishia uongozi kwenye kundi hilo,Mashabiki wanaofurika Uwanja wa Benjamin Mkapa wamekuwa nguzo kubwa, wakipeperusha bendera na kuunda mazingira ya presha kwa wapinzani.
Katika kundi A Harambee Stars wamechukua uongozi wa Kundi A kwa alama 7 baada ya mechi tatu,Ushindi muhimu wa 1–0 dhidi ya RD Congo na ushindi mwingine wa 1–0 dhidi ya Morocco umeweka Kenya mbele.Sare ya 1–1 dhidi ya Angola haijapunguza kasi ya vijana ambao sasa wanatazamia hatua ya robo fainali kwa matarajio makubwa, Mashabiki wa Nairobi wamesifu umoja na nidhamu ya wachezaji, wakisema “Safari hii tunataka kombe libaki Afrika Mashariki.”
Kundi C The Cranes wameonyesha makucha yao katika Kundi C, wakipata ushindi wa 3–0 dhidi ya Guinea na 2–0 dhidi ya Niger zimewaweka kileleni wakiwa na alama 6 baada ya mechi tatu huku wakipoteza mchezo mmoja dhidi ya Algeria kwa sasa Wamebaki na mchezo mmoja mkononi, lakini tayari wanaonekana kuwa na tiketi ya robo fainali.
Mashindano ya CHAN 2024 yameweka rekodi ya ushirikiano wa Afrika Mashariki, huku wenyeji wakitumia vyema uwanja wa nyumbani, Kilele cha hatua ya makundi kinatarajiwa wiki ijayo, na tayari vyombo vya habari vya kimataifa vinataja huu kama “mshikemshike wa kihistoria” kwa kanda hii.
Iwapo mwenendo huu utaendelea, kuna uwezekano mkubwa wa kuona Afrika Mashariki ikitoa bingwa wa CHAN 2024, jambo ambalo lingekuwa historia kubwa kwenye ramani ya soka la bara la Afrika.
0767915473.
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment