WENYEJI CHAN 2024 VICHWA CHINI

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa stars) na Kenya ambao ni wenyeji wa mashindano ya CHAN wameondoshwa kwenye michuano hiyo katika hatua ya robo fainali baada ya kupoteza michezo yao wakiwa kwenye ardhi ya nyumbani kwenye michezo iliyopigwa Agosti 22 katika uwanja wa Benjamin Mkapa na Moi International Sports Center.

Taifa Stars walikubali kichapo Cha bao Moja kwa bila katika mchezo uliokuwa wa kasi na kushambuliana kwa zamu , ambapo bao la Morocco likiwekwa kimiani na Oussama Lamlioui 65' ambalo lilikuwa bao pekee lililo wapeleka nusu fainali na kuidondosha stars.

ikumbukwe kuwa huo unakuwa mchezo wa kwanza kwa Tanzania kupoteza tangu mashindano yaanze ambapo katika hatua ya makundi hawakupoteza mchezo wowote huku wakiibuka vinara wa kundi B wakiwa na alama 10, lakini ubora Morocco uliamua hatma ya stars katika michuano hiyo.

Hii ni mara ya tatu kwa stars kushiriki mashindano hayo na ni ni kwa mara ya kwanza kufikia hatua ya robo fainali kitu ambacho hawajawahi kufanikiwa, hatua hii inaonyesha kukua kwa soka la Tanzania Kwa kuwa na muendelezo mzuri katika michuano ya kimataifa.



HARAMBEE STARS WAONDOSHWA KWA MIKWAJU YA PENALTY

Timu ya kenya (Harambee Stars) imeshangazwa na vijana kutoka Madagascar baada ya kuondoshwa kwa matuta baada ya dakika 120 kutamatika kwa sare ya 1-1, Harambee Stars ndio walikuwa wakwanza kuliona lango mapema kipindi Cha pili kupitia kwa Alphonce Ominja 48' na baadae Madagascar wakasawazisha kupitia Fenohasina Razafimaro 69' kwa mkwaju wa penati na mchezo kutamatika kwa sare.

Katika mikwaju ya penati Madagascar wali ibuka kidedea kwa ushindi wa mikwaju 4-3, na kuwaondosha wenyeji mbele ya mashabiki wao lukuki na kufuzu hatua ya nusu fainali katika mashindano hayo.

Washabiki wa soka nchini Kenya hawakutarajia kuondoshwa na Madagascar lakini mpira hauna mwenyewe , hatua hiyo ulikuja baada ya Tanzania kuwafunga Madagascar bao 2-1 katika mchezo wa kundi B , kitu ambacho kiliwaaminisha wa Kenya kuwa kwao utakuwa mteremko lakini haikuwa hivyo.

Sasa tambo za Tanzania na Kenya mtandaoni zimekwisha baada ya Timu zote ambao ni watani na majirani kuondoshwa katika hatua ya robo fainali na kwasasa muwakilishi pekee aliye salia katika michuano hiyo ni Uganda ambaye anatarajia kumenyana na Senegal , swali ni je, Uganda wataiheshimisha Afrika Mashariki au wata wafuata Kenya na Tanzania? majibu yatapatikana baada ya mchezo.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments