WAARABU WABISHA HODI KWA MZIZE

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

KLABU ya Espérance Sportive de Tunis kutoka Tunisia inatajwa kuwa mbioni kuwasilisha ofa rasmi kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa Yanga SC, Clement Mzize mwenye umri wa miaka (21).

Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyanzo vya kuaminika vya Yanga, muda wowote kuanzia sasa, Esperance wanatarajiwa kupeleka maombi rasmi ya kutaka kuinasa saini ya kinda huyo hatari anayeng’ara katika Ligi Kuu nchini na katika michuano ya kimataifa.

Hata hivyo, Yanga tayari wamekataa ofa ya $600,000 (dollar laki sita za kimarekani) kutoka kwa Al Masry ya Misri, wakieleza kuwa kiwango hicho cha fedha hakitoshelezi thamani ya mchezaji huyo kwenye soko la Afrika kwa sasa.


Inaelezwa kuwa uongozi wa Yanga uko tayari kupokea kiasi cha kuanzia dollar za kimarekani 800,000 hadi $900,000 ili kuachana rasmi na huduma ya mshambuliaji huyo anayetazamwa kama mmoja wa vipaji bora vya kizazi kipya cha soka la Tanzania.

Mzize ameonyesha kiwango bora msimu uliopita na kuibuka kuwa mmoja wa wachezaji muhimu wa kikosi cha Yanga, jambo lililowavutia mawakala na vilabu kadhaa kutoka nje ya nchi.

Endapo ofa ya Esperance itakubalika, basi dili hilo linaweza kuwa moja ya uhamisho mkubwa zaidi kwa mchezaji wa ndani ya Tanzania kwa kipindi cha hivi karibuni, kinachosubiriwa ni klabu ya Esperence kuwasiliaha ofa mezani na kufanya Dili.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments