Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Klabu ya Manchester United inaendelea na mawasiliano ya karibu na Brighton & Hove Albion kwa lengo la kumsajili kiungo chipukizi wa Kimataifa wa Cameroon, Carlos Baleba, huku mchezaji huyo akionyesha nia ya kujiunga na mashetani wekundu.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyanzo vya karibu na klabu hizo, United inatarajia kuwasilisha ofa ya awali kwa Brighton ili kujaribu kufanikisha dili hilo, Hata hivyo, hali inaonekana kuwa ngumu kwani Brighton hawana mpango wa kumuuza nyota huyo mwenye kipaji kabla ya mwaka 2026.
Mashabiki wa United wana hamu kuona usajili huo ukikamilika, huku taarifa zikibainisha kuwa klabu hiyo inaweza kutumia fedha zitakazopatikana kutokana na mauzo ya wachezaji wake akiwemo Alejandro Garnacho, Jadon Sancho na Antony ili kufanikisha dili hilo.
Aidha, masharti binafsi kati ya Baleba na Manchester United hayatarajiwi kuwa kikwazo iwapo makubaliano ya ada ya uhamisho kati ya klabu hizo mbili yatapatikana.
Iwapo usajili huu utatimia, Baleba anatarajiwa kuongeza nguvu kubwa katika safu ya kiungo ya Manchester United, ambayo imekuwa ikihitaji maboresho makubwa kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu ya England.
0767915473
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment