Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Mashabiki wa soka duniani wameendelea kushuhudia msururu wa matokeo mabovu ya Manchester United baada ya klabu hiyo kongwe ya England kutolewa kwenye michuano ya Kombe la Carabao na timu ya daraja la nne, Grimsby Town.
Katika mchezo huo uliochezwa usiku wa jana, Grimsby waliwaduwaza mashabiki kwa kuanza kupata mabao mawili kupitia kwa Charles Vernam dakika ya 22 na Warren dakika ya 30, Manchester United walirejea baadae kipindi cha pili na kusawazisha mabao kupitia kwa Bryan Mbeumo dakika ya 75 na Harry Maguire dakika ya 89.
Mchezo ulimalizika kwa sare ya 2-2 katika muda wa kawaida, na hivyo kuingia hatua ya mikwaju ya penalti, ambapo Grimsby Town wakapata ushindi kwa mikwaju 12-11, ushindi uliowapeleka hatua inayofuata huku Manchester United wakiondoshwa mapema.
Grimsby Town, ambayo inashiriki Ligi Daraja la Nne (League Two) nchini England, imeandika historia kwa kuitoa United, Ushindi huu umetafsiriwa na wachambuzi kama kipigo kinachoendeleza msururu wa matokeo yasiyoridhisha kwa Manchester United msimu huu, jambo linaloibua maswali makubwa kuhusu mustakabali wa kikosi hicho na benchi la ufundi.
Hofu imeanza kutanda kwa kocha wa kikosi hicho Ruben Amorim kuwa huenda akawa kocha wa kwanza kufungashiwa mizigo katika ligi England baada ya kuwa na matokeo yasiyo ridhisha kwani mpaka sasa kwenye michezo miwili ya EPL amepoteza mchezo mmoja na sare Moja pia kaondolewa Mashindano ya Carabao.
Mchezo uliopo mbele Yao ni Agosti 30 dhidi ya Burnley katika dimba old Trafford, mchezo huo utampa kocha huyo tafakari mpaya kuhusu muskabali wa klabu na yeye mwenyewe klabuni hapo. Swali ni je Amorim atafanikiwa kufika krismas akiwa na United? Matokea ya michezo inayofuata itatoa taswira ya kocha huyo klabuni hapo.
0767815473,
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment