UGONJWA WA KURUHUSU MABAO WAENDELEA KWA BARCELONA

 


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Barcelona waliibuka na Ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Levante, katika mchezo wa raundi ya pili uliopigwa kwenye uwanja wa Estadio Ciudad de Valencia Agosti 23, 2025, Ushindi huo unawafanya kufikisha alama sita , lakini hofu imekuja baada ya tatizo lao kwenye safu ulinzi kuonekana kuwa dhaifu.

Katika mchezo huo , Barcelona walijikuta wakiruhusu bao la mapema dakika ya 15 kupitia Romero kabla ya Morales kuongeza la pili kwa mkwaju wa penalti dakika ya 45+7, Matokeo hayo yaliwaacha Barcelona wakionekana kuyumba huku safu yao ya ulinzi ikishindwa kudhibiti mashambulizi ya Levante.

Hata hivyo, kipindi cha pili kilileta mabadiliko kwa Barcelona baada ya Pedri kusawazisha dakika ya 49, na Ferran Torres kuongeza bao la pili dakika tatu baadaye, na bao la Ushindi lilipatikana dakika ya 90+1 pale Elqezabal wa Levante alipofunga bao la kujifunga na kuihakikishia Barcelona alama tatu muhimu.

Licha ya ushindi huo, mashabiki wa Barcelona bado hawajaridhishwa kutokana na timu yao kuendelea kuruhusu mabao mepesi, hali inayoweza kuathiri malengo yao ya kutwaa ubingwa msimu huu, Kocha wa Barcelona amesema kikosi chake kitazidisha juhudi kurekebisha makosa ya ulinzi ili kuepuka presha kwenye michezo inayofuata.

Hali hiyo inakuja baada ya msimu uliopita timu hiyo kuruhusu mabao mengi katika michezo yao kitu ambacho wataalamunwa soka walisema kuwa kilipelekea kuwanyima Kutwaa ubingwa wa UEFA baada ya kutolewa hatua ya nusu fainali na Inter Milan kwa kuruhusu mabao Saba na kufunga mabao sita katika michezo yote miwili, hali ambayo iliwafanya kuondoshwa kwa Jumla ya kufungwa mabao (7-6).

Ugonjwa huo unaonekana kuwa bado haujapatiwa ufumbuzi kitu ambacho kitakuja kuwagharimu kwenye michezo dhidi ya timu zenye safu imara ya ushambuliaji, hali hii sasa inaibua mjadala mpana miongoni mwa wachambuzi wa soka Hispania, wakihimiza Barcelona kurekebisha mapema tatizo la ulinzi kabla ya michezo migumu iliyo mbele.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments