UGANDA YAFUFUA MATUMAINI KUSONGA MBELE CHAN 2024


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Timu ya Taifa ya Uganda imefufua matumaini yake ya kusonga mbele kwenye michuano ya CHAN 2024 , baada ya kuibuka na ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Guinea, kwenye mchezo uliopigwa jana uwanja wa Mandela stadium Kampala.

Katika pambano hilo, Uganda ilionyesha ubora wa hali ya juu licha ya kuwa na umiliki mdogo wa mpira (41%) ikilinganishwa na Guinea (59%), lakini uwezo wa wawachezaji hao katika kutengeneza nafasi na kutumia ulikuwa na usahihi wa Hali ya juu.

Mabao ya Uganda yaliwekwa kambani dakika ya 31 na Mpande, kabla ya Allan Okello kuongeza bao la pili kupitia mkwaju wa penalti dakika ya 62, Ahimbisibwe alihakikisha pointi zote tatu zinabaki mikononi mwa Uganda kwa kufunga bao la tatu dakika ya 89.


Katika mchezo huo nyota alikuwa Allan Okello, ambaye alitoa mchango mkubwa kwenye ushindi huo, Uganda walipiga jumla ya mashuti 12, manne kati ya hayo yakiwa yamelenga lango, huku Guinea ikipiga mashuti 6 pekee na mawili tu yakilenga lango.

Ushindi huo unaipa Uganda nafasi nzuri ya kupenya hatua ya makundi, huku wakiwa Hali ya juu kuelekea michezo inayofuata ili kulinda heshima ya uenjeji waliyo nayo, Mashabiki wa Uganda sasa wana matumaini makubwa kuwa timu yao inaweza kufika mbali katika mashindano haya

 katika kundi C mapema uliopigwa mchezo kati ya Algeria na Afrika kusini ambapo mpaka dakika tisini zinakamilika timu hizo zilitoshana nguvu kwa kufungana bao Moja moja, mpaka sasa kwenye kundi hilo kinara anasalia kuwa Algeria alama nne, akifutaiwa na Uganda alama 3, Guinea alama 3, wote wakiwa na michezo miwili huku Afrika kusini wakiwa na alama Moja mchezo mmoja na Niger ndio wakiwa wanabuluza mkia.



0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments