Timothy Lugembe,
LIVERPOOL VS ALEXANDER ISAK
Klabu ya Newcastle United inayo shiriki ligi kuu nchini England inatarajia kupokea ofa mpya kutoka kwa klabu ya Liverpool juu ya usajili wa mshambuliaji wao hatari Alexander Isak (25) baada ya mchezo wa leo kati ya timu hizo.
Hatua imekuja baada ya mchezaji huyo kugomea kubaki kabisa klabuni hapo na matamanio yake yamekuwa ni kujiunga na majogoo hao.
TOTENHAM VS NICO PAZ & SAVINHO
Totenham hotspurs ya nchini England imewasilisha ofay a pauni milioni 43 kwaajili ya kumsajili kiungo raia wa Argentina na klabu Como Nico Paz (20) lakini klabu hiyo ya nchini Italia imekataa ofa hiyo imesisitiza kuhitaji kiasi cha pauni milioni 60.
Pia spurs wako kwenye harakati za kumnasa winga wa Manchester City Savinho kama chaguo lao la kwanza baada ya kushindwa kufanikisha kumsajili Eberechi Eze ambaye amejiunga na washika mitutu wa London The gunners, spurs wametenga kitita cha pauni milioni 60 ili kuinasa saini ya winga huyo ambaye ameonesha matamanio ya kujiunga na klabu hiyo.
MANCHESTER UNITED VS SENNE LAMMENS
Manchester United wapo hatua za mwishoni kukamilisha usajili wa golikipa wa Royal Antwerp Senne Lammens kwa dau la Euro 25m, golikipa huyo raia wa ubelgiji tayali ameshakubaliana na klabu kuhusu maslahi yake bifasi kinacho subiriwa ni vilabu hivyo kufikia makubaliano.
Dirisha hilo linatarajiwa kufungwa septemba 1,2025, klabu nyingi msimu huu zinafanya usajili kwaajili ya kutengeza kikosi kipana ambacho kitakabiliana na hali za majeruhi ambazo huzisumbua timu hizo kila ifikapo katikati ya msimu ambapo wachezaji muhimu hupata majeraha na kusababisha baadhi ya timu kuporomoka kwa kiwango na kushindwa kufanya vizuri.
Hii imesababishwa na wachezaji wengi kukosa muda wa kupumzika katika msimu uliopita kufuatia mfululizo wa mashindano , sajili hizi zinazo endelea nikwaajili ya kuhakikisha baadhi ya wachezaji wanapata mapumziko kwa kucheza muda mchache ili kuepuka majeraha yatakayo igharim timu.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment