Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Uongozi wa klabu ya Simba sc rasmi imevunja ukimya baada ya maswali ya muda mrefu kuhusu uwepo wa tamasha lao la kila mwaka, sasa ni rasmi ‘Simba day’ ipo na itafanyika septemba 10 mwaka huu kwenye dimba la Benjamin Mkapa , Dar es laam.
Tamasha hilo hufanyika tarehe nane kila mwaka lengo likiwa ni kutambulisha kikosi na benchi la ufundi, lakini kwa mwaka huu tamasha hilo limepelekwa mbele kwa sababu ya mwingiliano wa ratiba kutokana na kuwepo kwa mashindano ya CHAN yanayo fanyika nchini huku timu ya Taifa stras ikiwa ni mshiriki mmoja wapo kitu ambacho kimelisogeza tamasha hilo kubwa Afrika Mashariki na kati mbele.
Mpaka sasa timu hiyo ipo nchini Misri ikiendelea na maandalizi kuelekea msimu mpya wa mashindano ambapo baadae itarejea nchini kwaajili ya tamasha hilo huku likiambatana na mchezo wa kirafiki ambao ni moja wapo ya sehemu ya tamasha.
Mashabiki wa klabu ya Simba wameonyesha furaha yao baada ya kutangazwa kwa tamasha lao huku wakisema kuwa tamasha hilo limeshakuwa utamaduni kwao hivyo licha ya kusogezwa mbele bado kwao haijaathiri chochote wanacho subiria ni siku ifike wakaiunge mkono timu yao.
0767915473,
Lugembetimothy01@gmail.com
Post a Comment