TAIFA STARS TIMU YA KWANZA KUFUZU ROBO FAINALI

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Timu ya Taifa ya Tanzania( Taifa stars) imekuwa timu ya kwanza kufuzu hatua ya robo fainali katika michuano ya CHAN2024 baada ya hapo jana kuibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Madagascar kwenye dimba la Benjamin Mkapa Dar es Laam.

Katika mchezo huo mabao ya Stars yaliwekwa kambani na mshambuliaji Clement Mzize dakika ya 13’, 20’ huku bao lakufutia machozi kwa upande wa Madagascar likifungwa na Razafimahatana dakika ya 34, licha ya kumiliki mpira nyuma ya wpinzani wao, stars walipiga jumla ya mashuti 14 na manne kati ya hayo ndio yaliyo lenga lango na kuzalisha goli mbili, kwa upande wao Madagascar walipiga jumla ya mashuti 12, huku mawili pekee yakilenga lango na kuzalisha bao moja.

Huo unakuwa ni mchezo wa tatu kwa stars huku wakiwa wamevuna alama zote Tisa na kuongoza kundi B kwa sasa timu hiyo inahitaji alama moja tu ili kujihakikishia kuongoza kundi hilo wakati wakiwa wamesalia na mchezo mmoja dhidi ya Jamuhuri ya Africa ya kati.

Hatua hii inazidi kudhihirisha ubora wa ligi kuu Tanzania bara huku wadau na mashabiki wa soka nchini wakisema kuwa hatua za mtoano ndizo zitakuwa kipimo kikubwa na cha mwisho kuwapima wachezaji wa timu hiyo kwani katika hatua hiyo watakabiliana na vigogo wa mpira barani Afrika , lakini Imani iliyopo ndani ya WaTanzania ni kuwa watafanya vizuri na kuishangaza Afrika.

Baada ya mchezo wa jana mpaka sasa kundi linasoma kama ifuatavyo.



0767915473.

Lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments