Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Mashabiki wa soka nchini Tanzania na barani Afrika kwa ujumla wanatarajia kushuhudia pambano la kusisimua la ufunguzi leo usiku kati ya timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) dhidi ya Burkina Faso katika michuano ya CHAN 2024, Mchezo huu muhimu unatarajiwa kuchezwa katika dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, kuanzia saa 2:00 usiku.
Huu ni miongoni mwa michezo ya hatua ya makundi ya michuano hiyo inayohusisha wachezaji wanaocheza katika ligi za ndani pekee,Tanzania inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na matarajio makubwa ya kufanya vizuri mbele ya mashabiki wake.
Kocha mkuu wa Taifa stars Hemed Suileman amesema wako vyema kwaajili ya mchezo kuanzia wachezaji na benchi la ufundi kwa hujumla huku lengo likiwa ni kushinda mchezo na kubakisha kikombe nyumbani kama ilivyo hamu ya Mashabiki wa soka nchini, pia amewatoa wasisi Mashabiki wa soka nchini kwa kuwahakikishia kuwa wamejiandaa vya kutosha na watafanya vizuri.
Golikipa wa stars Aishi Manula amesema kuwa kiu Yao kama wachezaji ni kuhakikisha wanaanza vizuri katika mchezo wao wa kwani ni mchezo wakwanza na wa ufunguzi kwa kuzingatia wa Tanzania wamesafiri kutoka maeneo tofauti tofauti watapambana ili kupata ushindi.
Kwa upande wa Burkina Faso, ambayo ni timu yenye uzoefu mkubwa katika mashindano ya kimataifa, haitakuwa mpinzani wa kubezwa, Kikosi hicho kinatarajiwa kuonyesha kandanda la ushindani mkubwa, hali inayowapa mashabiki sababu ya kutarajia burudani ya hali ya juu.
Jeshi la polisi na vyombo vya usalama vimehakikisha kuwa maandalizi yote ya kiusalama yamekamilika kwa ajili ya mchezo huo mkubwa, Vilevile, tiketi za kuingia uwanjani zilianza kuuzwa mapema wiki hii na mashabiki wameendelea kumiminika kwa wingi kuunga mkono Taifa Stars.
CHAN 2024 imeendelea kuwa jukwaa muhimu la kuonyesha vipaji vya wachezaji wa ndani, na kwa Tanzania, ni fursa adhimu ya kuonyesha ubora wa soka la ndani na kuinua morali ya vijana wanaowakilisha taifa.
0767915473.
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment