SPURS WAZIDI KUIMARISHA KIKOSI CHAO, WAMNASA XAVI SIMONS

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Klabu ya Tottenham Hotspur imetangaza rasmi kukamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji chipukizi Xavi Simons, akitokea RB Leipzig ya Ujerumani, baada ya makubaliano baina ya timu hizo kufikiwa.

Kwa mujibu wa taarifa dili hilo limekamilika kwa ada ya uhamisho ya €60 milioni, kiasi ambacho kilifikiwa baada ya majadilino kati ya pande zote mbili, tayari nyaraka zote muhimu zimesainiwa kati ya mchezaji na klabu na sasa Xavi Simons ni mchezaji halali wa Spurs.

Mkataba huo ni wa muda mrefu, ambapo Xavi atasalia Tottenham hadi Juni 2030, huku kukiwa na kipengele cha kuongeza miaka miwili zaidi ambacho kitamuwezesha kusalia klabuni hapo hadi 2032 endapo kila kitu kitaenda sawa.

Aidha, mchezaji huyo tayari ameshakamilisha vipimo vya afya, na taarifa zinaonyesha kila kitu kipo sawa na kinachosubiriwa ni kutangazwa tu rasmi na miamba hiyo ya London.

 Hatua hii inafanya Spurs kuvunja mipango ya wapinzani wao wakubwa, kwani awali kulikuwa na taarifa zikidai Chelsea walikuwa karibu kumnasa Xavi Simons, lakini hatimaye mchezaji huyo amechagua kuvalia jezi nyeupe za London Kaskazini.

Mashabiki wa Tottenham wameshuhudia klabu yao ikipiga hatua kubwa sokoni, na ujio wa Xavi unatazamwa kama sehemu ya mpango wa muda mrefu wa kuijenga Spurs kuwa na kikosi cha ushindani mkubwa barani Ulaya.

Usajili huo unaenda kuimarisha kikosi cha spurs ambacho kinaonekana kuanza vizuri ligi huku ikiimarisha zaidi na mashindano mengine makubwa ikiwemo UEFA CHAMPIONS LEAGUE.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com


0/Post a Comment/Comments