SOWAH KUIKOSA NGAO YA JAMII

Timothy Lugembe ,

Mwanakwetusports.

Mshambuliaji mpya wa Simba SC, Jonathan Sowah, hatoshiriki katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya watani wa jadi Yanga SC, mchezo unaotarajiwa kuchezwa Septemba ,2025 katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Sowah ataukosa mchezo huo kwa sababu ya adhamu ya kadi nyekundu aliyooneshwa wakati akiichezea Singida Black Stars katika fainali ya michuano ya Kombe la CRDB dhidi ya Yanga SC, ambapo Singida walipokea kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa miamba hiyo ya Kariakoo, huku mshambuliaji huyo akitolewa nje kwa kadi nyekundu kutokana na utovu wa nidhamu katika mchezo.

Kwa mujibu wa kanuni za Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB), adhabu ya mchezaji huendelea hata kama amehamia klabu nyingine ilimradi tu mashindano yote yako chini ya usimamizi wa chombo kimoja, hii inamaanisha kwamba mchezaji huyo atalazimika kuitumikia adhabu yake katika mchezo wa Ngao ya Jamii, licha ya kuhamia Simba SC.

Mchezo huo sasa unasubiriwa kwa hamu , kwani licha ya kukosekana kwa Sowah lakini bado Kuna washambuliaji wenye uwezo usiopishana ambao ni Suleiman Mwalimu, na Steven Mukwala ambao wanatarajiwa kuingiza safu ya ushambuliaji ya Simba Sc.

0767915473

lugembetimothy01@gmail.com


0/Post a Comment/Comments