Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Staa wa kandanda kutoka Korea Kusini, Heung-min Son, ametangaza rasmi kuondoka Tottenham Hotspur, klabu aliyohudumu kwa kipindi cha zaidi ya miaka kumi, huku taarifa zikieleza kuwa yupo katika mazungumzo ya kujiunga na timu ya Los Angeles FC inayoshiriki Ligi Kuu ya Soka Marekani (MLS).
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mchezaji huyo, uamuzi wake umetokana na kutamani changamoto mpya katika maisha yake ya soka, "Nimeomba kuondoka Spurs,, Nimejitahidi kwa kila hali kuwapa mashabiki wangu furaha, lakini sasa ni muda wa kutafuta upepo mpya," alisema Son kwa hisia nzito.
Akizungumza kwa hisia ya uchungu, Son alikiri kuwa huu ndio uamuzi mgumu zaidi kuwahi kuufanya. “Nilifika London Kaskazini nikiwa kijana mdogo, lakini leo naondoka nikiwa mwanaume aliyepevuka,” alisema huku akibubujikwa na machozi katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika nchini Korea Kusini.
Son ameacha historia ya kipekee ndani ya klabu hiyo maarufu ya Ligi Kuu England, Katika kipindi chake cha miaka 10, amecheza jumla ya mechi 454, akifunga mabao 173 na kutoa asisti 101, Kwa sasa, mashabiki wa soka ulimwenguni wanamsubiri kwa hamu kuona mwelekeo mpya wa nyota huyo wa Asia, huku LAFC ikiwa mstari wa mbele kunasa saini yake.
Mazungumzo yako nzuri na Los Angeles FC kwa ajili ya kuhamia MLS, baada ya vilabu vya Saudi kuonyesha nia tangu Mei lakini yeye amechagua MLS ,(ligi ya Marekani).
0767917573.
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment