Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Klabu ya Simba SC imeendelea kuimarisha kikosi chake kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu ya NBC na mashindano ya kimataifa baada ya kutambulisha rasmi usajili wa kiungo na beki wa kushoto kutoka Guinea, Naby Camara (23).
Camara, ambaye anasifika kwa uwezo wa kucheza nafasi zaidi ya moja uwanjani, anakuja kuongeza nguvu na ushindani katika safu ya ulinzi na kiungo cha Wekundu wa Msimbazi, nyota huyo amecheza katika vilabu kadhaa barani Afrika na Asia, ikiwemo CS Sfaxien ya Tunisia na Al-Waab SC ya Qatar.
Ujio wake unatarajiwa kuleta chachu mpya kwenye kikosi cha Simba, ambacho kimeweka wazi dhamira ya kufanya vizuri katika ligi ya ndani na kufika hatua za juu kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.
Mpaka sasa klabu ya Simba imefikisha Jumla ya wachezaji 13 wa kigeni japokuwa wanaotakiwa kikosini ni wachezaji 12, kwa usajili wa Camara utaenda kumuondoa mchezaji mmoja wapo klabuni hapo huku asilimia kubwa zikiangukia kwa Mutale na Ateba kuwa wanaweza kupewa Thank you klabuni hapo.
Mashabiki wa Simba wamepokea vizuri taarifa ya usajili huo huku wakiamini kuwa mchezaji huyo atakuwa nguzo muhimu katika kikosi Chao kutokana na uwezo wake wakucheza nafasi zaidi ya Moja kiwanjani.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment