Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Klabu ya Manchester United imefanikiwa kufunga dili kubwa la usajili wa mshambuliaji matata Benjamin Sesko baada ya nyota huyo kupunguza madai yake ya mshahara ili kufanikisha uhamisho wake kutoka RB Leipzig.
Kwa mujibu wa ripoti kutoka kwa wachambuzi na vyanzo vya karibu vya klabu mshahara wa awali wa Sesko umepunguzwa makusudi ili kuirahisishia United kumaliza usajili huo, huku dili zima likitajwa kufikia €85 milioni (takribani shilingi bilioni 247.8 za KiTanzania).
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 tayari amewasili Carrington kwa ajili ya vipimo vya afya (medical), na anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka mitano na mashetani wekundu.
Dili hilo limewekwa wazi kuwa litahusisha vipengele maalum vya nyongeza ambavyo vinaifanya RB Leipzig kuwa na uhakika mkubwa wa kupokea kiasi chote cha fedha kilichoafikiwa, na Usajili huu unakuja wakati United ikihitaji kuongeza nguvu mpya katika safu ya ushambuliaji kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu ya England.
SESKO anayejulikana kwa kasi, nguvu na uwezo mkubwa wa kufunga mabao, anatarajiwa kuwa mchezaji imara kwaNye kikosi Cha United.
Mashabiki wa Manchester United sasa wana kila sababu ya kutabasamu, wakimkaribisha nyota mpya Old Trafford kwa matumaini makubwa ya kurejea kwenye ubora wa zamani.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment