Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Kiungo wa zamani wa klabu ya Simba SC, Sadio Kanoute, amekamilisha usajili wake ndani ya kikosi cha Azam FC kwa mkataba wa miaka miwili, Hatua hii inakuja baada ya mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Mali kukamilisha mazungumzo na klabu hiyo.
Kanoute, ambaye alijiunga na Simba mwaka 2021, alijipatia umaarufu kutokana nanamna ya uchezaji wake akiwa dimbani alikuwa hana masihara kwenye suala la ukabaji na kupelekea kubatizwa jina la (Putin) ,pia anauwezo wa kuzuia mashambulizi na kupandisha mashambulizi kwa usahihi, Katika kipindi chake akiwa Msimbazi, alisaidia timu kushinda mataji ya ndani na kufika hatua za juu kwenye mashindano ya kimataifa.
Uongozi wa Azam FC umemkaribisha mchezaji huyo, ukibainisha kuwa ni sehemu ya mpango wa kuimarisha kikosi chao kuelekea msimu wa 2025/2026 wa Ligi Kuu Tanzania Bara na michuano ya CAF.
Mashabiki wa soka wanatarajia kumuona Kanoute akishirikiana na nyota wengine wa Azam FC katika kutafuta mafanikio, huku klabu ikilenga kuvunja rekodi na kuleta ushindani mkali kwa Simba na Yanga SC.
Klabu ya Azam fc, sasa inajenga kikosi imara ambacho kitaleta ushindani si ndani tu bali hata kimataifa kikosi hicho kwa sasa kwenye eneo la kiungo kanoute ataenda kuungana na, Himid Mao, Mamadou Samake, Akaminko , Bajana na Fei Toto.
Kanoute ataanza mazoezi rasmi na wenzake wiki hii, tayari kwa maandalizi ya michezo ya kirafiki na michuano ya ligi itakayoanza hivi karibuni.
0767915473.
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment