RASMI ZIMBWE NI MWANANCHI

 


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Beki wakushoto mahiri wa zamani wa Simba SC, Mohamed Hussein (Zimbwe jr) sasa ni rasmi amejiunga na mabingwa wa kihistoria nchini Young Africans SC , katika usajili wa dirisha kubwa la msimu wa 2025/2026.

Kupitia taarifa iliyosambaa mitandaoni, mchezaji huyo anaonekana kuchagua makombe na medali, jambo ambalo linaashiria kuwa amejiunga na klabu yenye malengo ya kushinda mataji, pia kuimarisha kikosi hicho kuelekea mashindano ya kimataifa kwani anauzoefu mkubwa kwa kufika hatua ya robo fainali na nusu fainali kwenye mashindano ya vilabu Afrika.

Hatua hiyo pia inafungua ukurasa mpya katika maisha ya soka ya Zimbwe Jr, huku ukurasa wa Simba ukifungwa rasmi, na ukurasa mpya jangwani ukifunguliwa, jambo linalochukuliwa kama pigo kwa Simba SC lakini neema kwa klabu ya Yanga.

Ujio wa Zimbwe Jr, unaonekana kuongeza ushindani na kuimarisha safu ya ulinzi ya Yanga kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara na mashindano ya kimataifa ambapo kwenye mabeki wa pembeni ataungana na Boka , Mwenda na kwasi.

Mashabiki wa Yanga tayari wameonyesha furaha yao kwa usajili huo, wakiamini kuwa beki huyo atakuwa msaada mkubwa katika kuendeleza mafanikio ya klabu hiyo, hii sio mara ya kwanza kwa Yanga kuchukua mchezaji muhimu katika kikosi Cha Simba ikumbukwe hapo awali walisha mchukua Jonas Mkude , Clatous Chama na sasa wamemnyofoa Zimbwe jr.

Swali la kujiuliza je, nikwanini klabu Yanga wanamudu kuchukua wachezaji muhimu kutoka Simba , na kwanini Simba hawawezi kuwanyofoa vigogo kutoka Yanga, ni sababu za Kiuchumi au ni mapenzi binafsi?


0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments