Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Paris Saint-Germain (PSG) wamefanikiwa kutwaa taji la UEFA Super Cup kwa mara ya kwanza baada ya ushindi wa mikwaju ya penalti 4-3 dhidi ya Tottenham Hotspur, kufuatia sare ya mabao 2-2 katika dakika 90 za mchezo, mchezo uliopigwa kwenye dimba la Bluenergy Stadium, Udine nchini Italy.
Mchezo huo ulianza kwa kasi, ambapo Tottenham walipata uongozi kupitia van de Ven dakika ya 39, kabla ya Cristian Romero kuongeza bao la pili dakika ya 48, PSG walionekana kukosa mwelekeo kwa muda, lakini dakika za jioni walifanya maajabu , Lee Kang-in alipunguza pressure dakika ya 85, na Goncalo Ramos akasawazisha dakika ya 90+4, akiweka matokeo sawa na kupeleka mchezo kwenye penalti.
Katika hatua ya mikwaju, PSG walionyesha utulivu na umakini mkubwa, wakifunga mikwaju minne , huku Tottenham wakipata mikwaju mitatu.
Kwa mujibu wa takwimu, PSG walimiliki mpira kwa asilimia 74 dhidi ya 26 za Tottenham ,wakipiga mashuti 12 huku matatu pekee yakilenga lango. Tottenham walipiga mashuti 13, na matano yakilenga lango .
Ushindi huo ni muendelezo mzuri kwa klabu ya PSG baada ya msimu uliomalizika kufanya vizuri kwa Kutwaa Mataji makubwa kama UEFA , Taji la ligi kuu ufaransa, pia walifanikiwa kushika nafasi ya pili katika mashindano ya vilabu ya dunia.
Kwa mafanikio hayo wanayozidi kuyapata mabingwa hao wa Ufaransa yanatengeneza njia na ushawishi wa mshambuliaji wa timu hiyo Ousmane Dembele Kutwaa tuzo ya mchezaji Bora wa dunia ( Ballon d' Or) dhidi ya wapinzani wake wa karibu miongoni mwao ni makinda kutoka FC Barcelona Lamine YAMALI na Pedri.
Kwa ushindi huu, PSG wameandika historia kwa kunyanyua taji la UEFA Super Cup kwa mara ya kwanza na kuonesha dhamira yao ya kulitawala soka la ulaya .
0767915473.
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment