PAZIA LA EPL LEO KUFUNGULIWA RASMI


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Mchezo wa ufunguzi ligi kuu ya Uingereza ( Community Shield) unatarajiwa kufanyika leo majira ya saa 11:00 jioni kwa saa za Afrika mashariki ambapo mchezo huo utawakutanisha klabu ya Liverpool dhidi ya crystal palace katika uwanja wa Wembley.

Livepool ambao ni mabingwa wa ligi kuu nchini humo wanakutana na palace ambao ni mabingwa wa kombe la FA ,mchezo huu ni kiashiria Cha kufunguliwa rasmi kwa pazia la ligi hiyo huku michezo rasmi itaanza kutimua vumbi agosti 15.


Kila timu inatazamia kuuanza msimu vizuri kwa kufungua kabati la makombe na taji hilo, mchezo unatarajiwa kuwa mgumu kwa pande zote mbili huku asilimia kubwa za ushindi zikilalia kwa Liverpool kutokana na usajili walio ufanya katika dirisha hili.

Swali ni je, Liverpool wataanzia pale walipo ishia msimu ulio pita na je, Palace watafanikiwa kumzuia Liverpool na kuuanza msimu kwa taji ? majibu yatapatikana baada ya mchezo.

0767915473.

Lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments