Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Klabu ya Manchester City ipo kwenye mazungumzo ya karibu na klabu ya Paris Saint-Germain (PSG) kuhusu kumsajili kipa wa kimataifa wa Italia, Gianluigi Donnarumma.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyanzo vya karibu na uongozi wa miamba hiyo ya Ulaya, City na PSG wanakaribia kufikia makubaliano ambayo yanaweza kumpeleka Donnarumma Etihad kwa ada inayokadiriwa kati ya Euro30 hadi 35 milioni.
Hata hivyo, mpango huu unatajwa kutimia tu endapo kipa namba moja wa sasa wa City, Ederson Moraes, ataondoka katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi, Ederson amekuwa mhimili mkubwa wa safu ya ulinzi wa mabingwa hao wa England tangu alipojiunga nao mwaka 2017, lakini tetesi za kuondoka kwake zimeanza kushika kasi.
Donnarumma, mwenye umri wa miaka 25, amekuwa mhimili wa PSG tangu alipojiunga mwaka 2021 akitokea AC Milan, na amejijengea heshima kubwa kutokana na uwezo wake wa kuokoa michomo ya hatari.
Iwapo dili hili litatimia, litakuwa ni moja ya usajili mkubwa wa makipa katika Ligi Kuu ya England na litampa kocha Pep Guardiola chaguo jingine thabiti la kulinda lango la kikosi chake.
Mashabiki wa City sasa wanasubiri kuona mustakabali wa Ederson kabla ya hatma ya Donnarumma kuungana na mabingwa hao wa Ulaya.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment