Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Klabu ya Simba SC imefanikiwa kumsajili rasmi kipa namba moja wa Taifa stars na JKT Tanzania, Yakoub Suleiman Ali mwenye umri wa miaka (25) baada ya mvutano wa muda mrefu na klabu yake ya zamani.
Taarifa kutoka ndani ya Simba zinaeleza kuwa uongozi wa wekundu wa Msimbazi ulikutana na changamoto kutokana na JKT kusita kumruhusu mchezaji huyo kuondoka kutokana na kuhitaji huduma yake, lakini jitihada za Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Mohamed Dewji “Mo”, hatimaye zimezaa matunda na kufanikisha usajili huo.
Yakoub Suleiman Ali anatajwa kuwa mmoja wa makipa bora wazawa kwa sasa katika Ligi Kuu ya NBC, akiwa na uwezo mkubwa wa kuokoa michomo na kuiongoza vizuri safu ya ulinzi, Imeelezwa kuwa kipa huyo ataungana rasmi na kikosi cha Simba baada ya kumalizika kwa michuano ya CHAN.
Usajili wa Yakoub unatarajiwa kuimarisha zaidi safu ya ulinzi ya Simba SC, ambayo msimu huu imeonyesha dhamira ya kuongeza nguvu katika kila idara ili kuhakikisha inarejesha ubingwa wa ligi na kufanya vizuri katika Ligi ya Mabingwa Afrika.
Sambamba na Hilo klabu ya Simba imefanikiwa kumnasa nyota mwingine kutoka JKT Wilson Nangu ambaye naye atajiunga na kikosi baada ya mashindano ya CHAN.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment