Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Klabu ya Yanga imefanikiwa kumbakiza mshambuliaji wao muhimu,Clement Mzize, baada ya pande zote mbili kufikia makubaliano mapya ya mshahara, Mchezaji huyo sasa atakuwa akilipwa shilingi milioni 40 kwa mwezi, huku mkataba wake ukibaki pale pale wa miaka miwili.
Mzize ameboreshewa maslahi yake baada ya kuwepo kwa timu kadhaa nje ya Tanzania zilizokuwa zikihitaji huduma yake miongoni mwa timu hizo ambazo zilijitokeza Moja kwa Moja kutumia ofa kwa klabu ni Esperence ya Tunisia na Al Massry ya nchini Misri lakini wananchi hawajaonyesha unyonge kumwachia kirahisi na badala yake wamembakisha kwa kumuaongezea mshahara.
Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zinaeleza kuwa kilichoongezwa ni kipengele cha malipo, lakini muda wa mkataba haujabadilishwa, hatua hii imekuja ikiwa ni mkakati wa Yanga kuhakikisha hawapotezi wachezaji muhimu kuelekea msimu ujao.
Katika soka Moja ya sajili bora ambazo hufanywa na klabu ni pamoja na kubakiza wachezaji mihiri katika timu, Yanga wameonyesha kuwa ni sehemu ya jambo hilo na wathibitisha ukubwa wao Kwa kuwa bakiza wachezaji muhimu kwenye timu akiwemo Pacome zouzoua, Max , na Mzize wachezaji ambao waliimbwa kuondoka lakini klabu imesimama imara na kuwabakisha kwa kuwaboreshea maslahi.
Yanga imeweka wazi dhamira yao ya kushindana katika ngazi ya kimataifa, jambo linalowafanya kuwa makini zaidi katika suala la usajili na uendelezaji wa kikosi chao, Viongozi wa klabu hiyo wamesisitiza kwamba hawako tayari kuachia mastaa wao nyakati hizi ambazo wanataka kujitangaza kimataifa.
Mashabiki na wadau wa soka nchini wameeleza kuwa hatua hiyo ya Mzize kuongezewa mkataba Jangwani itamuongezea thamani zaidi hasa akifanikiwa kuonyesha kiwango kizuri kwa msimu ujao na klabu inaweza kumuuza kwa bei kubwa na kupata faida.
Kwa makubaliano haya, mashabiki wa Yanga wana kila sababu ya kuendelea kuwa na matumaini makubwa msimu ujao, wakiamini timu yao itakuwa na nguvu mpya ya kushindana ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment