Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Bingwa mtetezi klabu ya Liverpool imeanza pale ilipoishia msimu ulioisha kwa kuendeleza ubabe wake katika Ligi Kuu nchini England baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Bournemouth katika dimba la Anfield.
Katika mchezo huo wa kwanza kwenye ligi hiyo Liverpool waliokuwa wakwanza kuliona lango mapema ambapo Mabao yao yalifungwa na Hugo Ekitike dakika ya 37, Cody Gakpo dakika ya 49, Federico Chiesa dakika ya 88 na Mohamed Salah aliyefunga dakika za nyongeza 90+4.
Bournemouth walipata mabao yao kupitia Antoine Semenyo aliyetikisa nyavu mara mbili dakika ya 64 na 76, lakini hayakutosha kuwanyima wenyeji alama zote tatu muhimu.
Kipindi cha kwanza Liverpool walionekana kutawala mchezo kwa umiliki wa mpira na mashambulizi ya mara kwa mara, hali iliyowalazimu wageni kujilinda muda mrefu, Bao la Ekitike liliwapa ujasiri huku Gakpo akiongeza mwanzoni mwa kipindi cha pili.
Hata hivyo, Bournemouth walijibu kwa nguvu kupitia Semenyo aliyeonyesha uwezo mkubwa kwa kufunga mabao mawili ya haraka na kuuweka,mchezo kwenye mzani sawa , Lakini Chiesa aliyeingia kipindi cha pili alihakikisha Liverpool inapata tena uongozi kabla ya Salah kumaliza mchezo kwa staili dakika za lala salama.
Kwa matokeo hayo, Liverpool wanakaa kileleni baada ya mchezo huo ambao ni wakwanza kwenye ligikuu England, huku wakisubiria michezo mingine ili kujihakikishia nafasi hiyo, huku kwa upande wa Bournemouth wakibaki kusaka matokeo bora zaidi ili kuepuka kuporomoka kwenye nafasi za chini.
Katika mchezo huo nyota mpya wa Liverpool Ekitike alifanya vizuri baada ya kufunga bao na kutoa pasi ya usaidizi wa goli (assist), na kufamfanya kuibuka kuwa mchezaji bora wa mchezo huo, na huu ni mchezo wake wa pili mfululizo kufumania nyavu baada ya kufunga katika mchezo wa Ngao ya hisani dhidi ya palace.
Michezo mingine inatarajiwa kuendeleza ili kukamilisha mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo swali ni je, nani kwa msimu huu anatwaa taji? au ni Liverpool atafanikiwa kutetea ubingwa ? majibu yatapatikana kadri ya michezo inavyo zidi kusonga mbele.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment