LIGI KUU NBC 2025/26 kUANZA SEPTEMBER 16



Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Bodi ya ligi Tanzania Bara imetangaza rasmi tarehe ya kuanza kwa ligi hiyo kupitia Afisa habari wake Karim Boimanda kwa kusema kuwa ligi itaanza rasmi tarehe 16, September mwaka huu.

 kwa msimu huu ligi hiyo imeonekana kuchelewa tofauti na misimu kadhaa nyuma hii ni kutokana na kuwepo kwa ratiba ya mashindano ya kimataifa (CHAN) amabayo yanahusisha wachezaji wanao cheza ligi za ndani amabapo timu ya taifa ya Tanzania ni mshiriki mmoja wapo wa michuano hiyo ambayo itaanza kutimua vumbi Agosti 2, na inafanya ligi hiyo kuchelewa ili kupisha timu ya Taifa na mashindano ya CHAN kwa ujumla.

Baadhi ya timu za za ligi kuu tayali zimekwisha anza maandalizi kuelekea msimu mpya ikiwa ni kujiweka tayali kwa mashindano ya ndani na nje ya nchi , timu kama Simba, Yanga na Azam zimekwisha anza maandalizi yao mapema kujinoa ili kuhakikisha wanafanya vizuri sio katika ligi ya ndani tu, bali kuhakikisha wanapeperusha bendera ya nchi kimataifa kupitia mashindano ya klabu bingwa na shirikisho.

Baada ya tarehe ya kuanza kwa ligi kutangazwa wadau na mashabiki wa soka nchini wameshauri kuwa bodi ya ligi ijitahidi kupanga ratiba vizuri ili kuepuka upanguaji wa mara kwa mara wa ratiba , kwa upande mwingine wameiomba ligi ifanye haki kwenye upangaji wa muda kwani vilabu nje ya Simba na Yanga zinapangiwa kucheza mpaka saa 8, lakini Simba na Yanga wamekuwa wakicheza kuanzia saa 10 , hivyo waomba mzani wa ratiba uwe wenye haki kwa timu zote.

Muda wowote bodi ya ligi watatangaza ratiba ya michezo kwa msimu ujao hivyo timu zizidi kufanya maandalizi ya kutosha kuelekea msimu mpya wa mashindano, ambapo kutokana na sajili mbali mbali ligi hiyo inazidi kuimarika na msimu ujao unatarajiwa kuwa wenye ushindani Zaidi.

0767915473,

Lugembetimothy01@gmail.com


0/Post a Comment/Comments