Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Timu ya Kenya (Harambee stars) imewashangaza wengi baada ya jana kuichakaza timu ya Taifa Morocco kwa 1-0, katika mchezo wa kundi A ulipigwa kwenye uwanja wa Moi International Sports Centre jijini Nairobi, nakuongoza kundi hilo huku wakibakiza mchezo mmoja kujihakikishia kufuzu.
Katika mchezo huo Harambee stars waliingia kama timu ya pili huku timuiliyopewa nafasi kubwa ya kushinda ilikuwa ni Morocco, mambo yalikuwa ndivyo sivyo baada ya Ogam 42’ kuifungia bao la uongozi harambee stars na bao pekee la ushindi mpaka dakika tisini zinakamilika.
Harambee stars wamedhihirisha ubora wao katika eneo la ulinzi baada ya kucheza kipindi cha pili chote wakiwa pungufu baada ya mchezaji wao Chris Erambo kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 45’, licha ya kuwa pungufu walifanikiwa kulinda bao hilo licha mashambulizi mfululizo kutoka kwa wapinzani lakini hawakuruhusu bao, ikumbuwe kuwa hata mchezo wao uliopita dhidi ya Angola walipata sare ya 1-1 licha ya kuwa na kadi nyekundu, kwa hali hii inaonyesha ubora wa Kenya eneo la ulinzi baada ya kumudu kucheza michezo miwili katika hali hiyo na kupata matokeo.
Katika hatua mchezo mwingine kwenye kundi A, timu ya Taifa ya Angola kuibuka na ushindi wa bao 2-1 mchezo ulio pigwa dimba la Nyayo Stadium, Nairobi Kenya
Katika mchezo huo Zambia ndio walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 73’ kupitia Chanda na baadae Angola kurudi kwa kasi na kupata ushindi kupitia mabao yaliyo fungwa na Kaporal 79’ 86’ nakuufanya mchezo kumalizika kwa angola kupata ushindi huo muhimu.
Baada ya michezo hiyo Kenya wanaongoza kundi wakiwa na alama saba huku nafasi ya timu wenyeji kufuzu robo fainali ikiwa kubwa ambapo mchezo wa mwisho watakutana na Zambia ambae hana alama yeyeyote.
0767915473,
Lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment