Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Timu ya taifa ya Uganda, moja ya wenyeji wa michuano ya CHAN 2024, imeshindwa kutendea haki uwanja wa nyumbani baada ya kubugizwa mabao 3-0 na Algeria katika mchezo wa kundi C, uliochezwa kwenye Uwanja wa Mandela, Kampala, Kipigo hicho kinaiweka Uganda katika historia ya kuwa timu ya kwanza mwenyeji kufungwa katika mashindano haya ya Afrika Mashariki baada ya Tanzania na Kenya kuanza na ushindi.
Katika mchezo huo Magoli ya Algeria yalifungwa na Ghezala dakika ya 36, Bentahar dakika ya 76 na Bayazid dakika ya 79, huku mchezaji wa Algeria Abderrahmane Meziane Bentahar akitangazwa kuwa Mchezaji Bora wa Mechi kwa mchango wake mkubwa uwanjani.
Licha ya Uganda kumiliki mpira kwa asilimia 46 na kufanya mashuti 11 (matatu pekee yakiwa golini), hawakuweza kutikisa makali ya Algeria waliotawala kwa asilimia 54 ya umiliki wa mpira na mashuti 10, huku matano yakilenga lango na matatu kuzaa matunda.
Katika mchezo mwingine ambao uliopigwa mapema Timu ya taifa ya Guinea imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Niger katika mchezo uliomalizika kwa ushindi uliotokana na bao pekee lililofungwa na Mohamed Bangoura dakika ya 48.
Bangoura ambaye alionesha kiwango bora uwanjani alitajwa kuwa Mchezaji Bora wa Mechi kutokana na mchango wake mkubwa, ikiwemo bao hilo muhimu lililoihakikishia Guinea pointi tatu muhimu.
Guinea walitawala mchezo kwa asilimia 52 ya umiliki wa mpira, huku wakipiga jumla ya mashuti 11, ambapo manne kati ya hayo yalienga lango huku Niger walipiga mashuti nane tu na kufanikiwa kulenga shabaha mara moja pekee
Baada michezo hiyo ya kundi C Kupigwa Algeria ndio anaongoza kundi akiwa na alama 3 na faida ya magoli matatu, huku Guinea wakishika nafasi ya pili wakiwa na alama 3 na goli moja nafasi ya tatu ikishikwa na Afrika kusini ambao Bado hawajacheza mchezo wao, lakini nafasi ya nne na Tano ni Uganda na Niger wakiwa hawana alama.
Mashabiki na wadau wasoka wanasubiria kuona mwenendo wa timu ya Uganda kama utabadilika au atatia aibu Kwa kuwa timu mwenyeji kuondoshwa mapema kwenye mashindano majibu yatapatikana baada ya michezo ya raundi zijazo Kupigwa.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment