KENYA NA MOROCCO WATEMBEZA KICHAPO KUNDI A


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Katika mashindano ya CHAN 2024 yanayo endelea kutimu vumbi katika nchi tatu za Afrika Mashariki yameendelea kushika kasi baada ya jana kupigwa michezo ya kwanza ya kundi A nchini Kenya kama kituo mojawapo ambapo mashindano hayo yanafanyika.

Katika mchezo wa mapema ambao uliwakutanisha wenyeji Kenya (Harambee stars) dhidi ya Congo DR ulimalizika kwa Kenya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 bao lililofungwa dakika ya 45+2 na mchezaji Austin Odhiambo na mpaka dakika tisini zinakamailika Kenya walishinda mchezo na kuwashangaza wengi amabao waliamini Congo angeshinda mchezo huo.

Mchezo huo ulikuwa niwakusisismua na wakasi kwa dakika zote tisisni huku timu zote zikishambuliana kwa zamu , licha ya Kenya kushinda mchezo huo lakini timu zote zilishambuliana kwa kupishana , takwimu zinaonyesha kuwa timu zote zilimiliki mpira kwa asilimia 50, ambapo congo walipiga jumla ya mashuti 20 huku yaliyo lenga yakiwa mawili, ambapo Kenya walipiga mashuti 8, yaliyolenga lango yakiwa mawili ambalo moja ndilo lilikuwa bao.

Mchezo mwingine wa kundi hilo uliwakutanisha Morocco dhidi ya Angola ambapo ilishuhudia Morocco wakiibuka na ushindi wa bao 2-0 ambapo mabao hayo yaliwekwa kimiani na Imad Riah 29’ na kinito 81’ amabaye alijifunga.

Katika mchezo hua licha Angola kupoteza lakini waliongoza kwa umili wa mpira na kuutawala mchezo kwa asilimia 59 dhidi ya 41 za wapinzani wao, katika mashuti walipiga mashuti 6 huku mawili yakilenga lango na Morocco walipiga mashutu 7, na matano yalilenga lango na kuzalisha magoli mawili.

Baada ya michezo hiyo kutamatika timu ya taifa ya Morocco inaongoza kundi hilo ikiwa na alama 3 na faida ya goli mbili, ikifuatiwa na Kenya alama 3 kwa faida ya goli moja na nafasi ya tatu ni Zambia ambaye bado hajacheza mwenye alama 0, na wanaobuluza mkia ni DR Congo na Angola ambao hawana alama .

Michezo inayofuata katiaka kundi A itapigwa Agosti 7 na 10, ambapo Angola atamenyana na Kenya, DR Congo atamenyana na Zambia huku agosti 10 itakuwa Kenya dhidi ya Morocco, swali ni je, wenyeji Harambee stars wataweza kuendeleza walipo ishia na kuvuka hatua ya kundi.


0767915473.

Lugembetimothy01@gmail.com


0/Post a Comment/Comments