Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Klabu ya Bayern Munich imefanikiwa kutikisa tena soko la usajili barani Ulaya baada ya kukamilisha dili la kumsajili mshambuliaji kutokea Chelsea, Nicolas Jackson.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi, mchezaji huyo amejiunga na miamba ya Ujerumani kwa mkopo wa msimu mmoja wenye thamani ya €15 milioni, huku kipengele cha kumnunua kikiwa kimewekwa kwa dau la kufikia €80 milioni ifikapo mwaka 2026 Ingawa kipengele hicho si cha lazima.
Chelsea nao hawajabaki nyuma, kwani wameweka sharti la sell-on clause, litakalowapa sehemu ya faida endapo Bayern watakubali kumnunua moja kwa moja hatua hiyo imewafanya mashabiki wa The Blues kuona klabu yao imecheza karata ya kibiashara kwa ustadi mkubwa.
Jackson, anayejulikana kwa kasi yake, nguvu na uwezo wa kumalizia nafasi, anatarajiwa kutua Bavaria leo hii akiambatana na wakala wake Ali Barat wa kampuni ya Epic Sports, ili kukamilisha vipimo vya afya na taratibu za mwisho za uhamisho huo.
Bila shaka, hatua hii imezidi kuonyesha jinsi Bayern wanavyopanga kwa makini kurejesha heshima yao barani Ulaya, wakati Chelsea nao wakibaki na matumaini ya kujipanga upya kwa nyota wengine waliobaki kikosini.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment