HII HAPA JEURI YA STARS KUWAONDOA MOROCCO ROBO FAINALI

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Mashindano ya (CHAN 2024) yanaendelea kushika kasi baada ya hatua ya makundi kutamatika rasmi Katika makundi A na B, ambapo timu za Kenya na Morocco wakifuzu Katika kundi A, huku kundi B ikiwa ni Tanzania na Madagascar, ambapo robo fainali hizo za kwanza zitapigwa Agosti 22, 2025.

 Taifa stars watamenyana na Morocco mabingwa mara mbili wa mashindano hayo, hatua hiyo imekuja baada ya Stars kumaliza kinara kundi B akiwa na alama 10, na Morocco akimaliza nafasi ya pili kundi A akiwa na alama 9, mchezo huu utapigwa dimba la Benjamin mkapa huku matumaini ya Stars kusonga mbele yakiwa makubwa kutokana na faida ya kucheza nyumbani mbele ya Mashabiki wake.

NINI KINAIPA JEURI STARS KUFUZU NUSU FAINALI

Kufanya vizuri kwa stars katika msimu huu wa mashindano kunaonyesha ni matunda na jitihada za muda mrefu katika kuandaa timu, ikumbukwe kuwa hii ni mara ya kwanza kwa timu hii kuvuna alama 10 na kuongoza kundi tangu mashindano haya yaanzishwe na ubora huu unachagizwa na ubora wa ligi ya Tanzania (NBC premier league) kwa kutoa wachezaji Wazuri na wenye viwango vya kushindana kimataifa.

Pili Stars katika kikosi chake kimesheheni nyota wenye uzoefu wa kucheza mashindano ya kimataifa na kufikia hatua za juu kabisa ikiwemo fainali mashindano ya vilabu huku wakiipata uzoefu kwa kucheza na timu vigogo barani Afrika kama Mamelod, National Al Ahaly, RS Berkane na timu nyinginezo nyingi, miongoni mwa wachezaji hao huto acha kuwataja Mohamed Hussein, Dickson Job, Ibrahim Bacca, Shomari kapombe, Yusufu Kagoma na Clement Mzize.

Tatu ni historia ya uwanja wa Benjamin mkapa hasa hasa inapo kuja Mechi na timu kutoka Uarabuni, katika kipindi Cha hivi karibuni hasa katika ngazi ya vilabu timu kubwa za Uarabuni kama vile Al Ahaly na Wydad imekuwa ngumu kuchomoka katika dimba Hilo licha ya ubora wao , hiyo unachagizwa na kauli mbiu kuwa kwa mkapa hatoki mtu.

Sapoti kutoka serikalini ambapo Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suruhu Hassan ameweka ahadi kubwa kwa timu hiyo , atatoa kitita cha Billioni 1 iwapo watafanikiwa Kutwaa taji hilo.

Siku zote historia zinawekwa na kuvunjwa Katika mchezo huo Tanzania anaingia kama timu ya pili kwa kuzingatia historia lakini itaingia kama timu yenye matumaini makubwa ya kusonga mbele kutokana na ubora wa kikosi chake na faida ya kucheza nyumbani.

Mashabiki wa Stars Sasa ni muda wa Kuvaa uzalendo kwa kujitokeza kwa wingi uwanjani na kushangilia kwa nguvu ili kuhakikisha historia inaandikwa na kombe kubaki nchini.


0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments