FADLU ATOA MSIMAMO KUHUSU USAJILI, ATAKA MSHAMBULIAJI MWENYE UWEZO WA ZIADA

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Kocha mkuu wa Simba SC, Fadlu Davids, amefunguka kuhusu mikakati ya kikosi chake kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu na michuano ya kimataifa, akibainisha kuwa bado wanahitaji mchezaji mwenye ubora wa juu atakayeleta tofauti kwenye safu ya ushambuliaji.

Kwa mujibu wa Davids, licha ya mchango mkubwa uliotolewa na Rais wa klabu hiyo, Mohammed Dewji, msimu uliopita Simba ilikosa mchezaji mwenye uwezo wa kubadilisha matokeo kwenye mechi kubwa, ikiwemo michezo ya fainali na dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga SC.

Kocha huyo amesema kuwa kumalizika kwa dirisha la usajili kunampa matumaini ya kupata mchezaji wa aina hiyo kupitia jitihada za viongozi wa klabu akiwemo Jayrutty, ili kuongeza makali ya kikosi hicho katika eneo la mwisho.

Davids amesisitiza kuwa lengo la Simba msimu huu ni kuwapiku wapinzani wao wa jadi, Yanga, ambao amekiri kuwa wamekuwa na ubora mkubwa wanapokutana kwenye michezo mikubwa.

Aidha, ameweka wazi kuwa Simba inalenga pia kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa, jambo linalohitaji wachezaji wenye kiwango cha juu na uzoefu wa kukabiliana na ushindani wa ngazi hiyo.

Mashabiki wa Simba bado wanamaswali kuhusu usajili ambao uliahidiwa na Moja ya mdhamini wao Jayrutty ambae aliahidi kusajili mchezaji mmoja atakae kuwa kipenzi Cha Mashabiki wa klabu hiyo lakini kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa msemaji wa timu hiyo Ahmed Ally amesema kuwa usajili wa mdhamini wao utaanza kutekelezwa mwezi disemba.

Swali ni je kwanini usajili usifanyike sasahivi kipindi ambacho kocha anahitaji huduma ya mchezaji mwenye uwezo wa ziada ? Na kwanini klabu isimpatie kocha anachokitaka ili kuepuka kumpatia lawama baadae? Kazi inabaki kwa uongozi wa Simba na benchi la ufundi kufanya maamuzi.

0767915473

lugembetimothy01@gmail.com


0/Post a Comment/Comments