Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Klabu ya Arsenal ipo hatua za mwisho kukamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji matata wa Crystal Palace, Eberich Eze (27), baada ya kufikia makubaliano ya maslahi binafsi na nyota huyo huku kila kitu kikienda sawa baina ya pande zote mbili.
Awali, mahasimu wao wa London Kaskazini, Tottenham Hotspur, walikuwa vinara katika mbio za kumsajili Eze na tayari walikuwa wamekubaliana maslahi binafsi , lakini Arsenal waliingia kwa kishindo na kutoa ofa kubwa zaidi ya £60m iliyoivutia Crystal Palace pamoja na mchezaji mwenyewe.
Hatua hiyo imezima ndoto za Spurs, na sasa mashabiki wa Arsenal wanaanza kujiandaa kumshuhudia kiungo huyo mwenye uwezo wa kucheza maeneo yote ya ushambuliaji akivalia jezi nyekundu na nyeupe msimu huu wa 2025/26.
Uamuzi wa Arsenal kumsajili Eze umechochewa na jeraha alilopata kiungo wao Kai Havertz, jambo lililowalazimu kutafuta mbadala wa haraka ili kuimarisha safu ya kati na kuongeza ubunifu katika eneo la ushambuliaji.
Mashabiki wa The Gunners wanaamini ujio wa Eze unaweza kuwa chachu ya safari yao ya kuelekea kutimiza ndoto ya kutwaa makombe makubwa msimu huu, huku kocha Mikel Arteta akitazamiwa kumpa nafasi kubwa katika kikosi chake cha kwanza kutokana na uzoefu wake katika ligi hiyo.
Kwa sasa kinachosubiriwa ni tangazo rasmi la Arsenal, ambalo litahitimisha rasmi usajili huu unaochochea msisimko mkubwa katika soka la Uingereza.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment