Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Arsenal imethibitisha kukamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji wa Kimataifa wa England, Eberechi Eze(27) ,anarejea kaskazini mwa London alikopitia katika akademi ya vijana ya Arsenal, kabla ya kung’ara na kujulikana kama moja ya vipaji hatari zaidi katika Ligi Kuu ya England akiwa na Palace.
Mchezaji huyo ametambulishwa Jana katika mchezo wa Arsenal dhidi ya Leeds united ambapo walishinda kwa bao 5-0, hata hivyo Usajili wa mshambuliaji huyo umechochewa na majeraha ya Kai Havertz katika mchezo wa kwanza dhidi ya Manchester United , Eze atavaa jezi namba 10 na ameungana na kikosi baada ya mchezo huo.
Mkurugenzi wa Michezo wa Arsenal, Andrea Berta, alisema kuwa mchezaji huyo atawasaidia kwa kutumia uzoefu wake wa kucheza na kuamua matokeo.
"Tunafurahia sana kumpata Eberechi, ni mchezaji mwenye ubunifu, nguvu na uzoefu mkubwa, anaweza kuamua matokeo ya mechi kubwa na tunaamini atakuwa msaada mkubwa kwa kikosi chetu."
Kocha Mkuu Mikel Arteta naye aliongeza kwa kuonyesha furaha yake huku akiwa na matarajio makubwa kwa mchezaji huyo kuwasaidia kufanya vizuri kutokana na kipaji na nidhamu yake.
"Tunafurahi kumsajili Eberechi, atatupa sura mpya kwenye safu ya ushambuliaji Kinachovutia zaidi ni juhudi na nidhamu yake katika safari ya soka ameonesha azma kubwa, na hiyo ndiyo tunayoitaka kwa kikosi chetu."
Mashabiki wa Arsenal wamesema kuwa usajili huo utaenda kuongeza nguvu katika eneo la ushambuliaji pia itaongeza rotation katika kikosi ili kupekana na majeruhi katika kikosi hicho jambo ambalo limekuwa likiwasakama misimu ya nyuma na kuwasababishia kuukosa ubingwa wa EPL.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment