DROO YA VILABU CAF TAYALI , VIGOGO TANZANIA WAANZIA HATUA YA AWALI



Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Droo ya michuano ya kalbu bingwa na shirikisho barani Afrika imefanyika Agosti 9, kuanzia majira ya saa saba mchana nchini Tanzania ambapo vilabu vilizofuzu kushiriki mashindano hayo kote Afrika tayali vimeshawafahamu wapinzani wao .

Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi kuanzia septemba 19-21 mwaka huu kwa raundi ya kwanza huku michezo ya marudiano ikitarajiwa kufanyika septemba 26-28 mwaka huu.

Katika droo hiyo upande wa klabu bingwa Simba Sc itamenyana na Gaborone United kutoka Botswana amabapo mchezo wakwanza utafinyika nchini Botswana na mchezo wa marudiano utafanyika nchini Tanzania, klabu ya Yanga Africa watakutana na klabu ya Wiliete Benguela kutoka nchini Angola ambapo nao wataanzia ugenini nchini Angola na kumalizia nchini Tanzania.

Kwa upande wa shirikisho klabu ya Azam fc imepangwa kucheza na Al Merriekh Bentui ya Sudani kusini huku mchezo wa kwanza ukifayika Sudani na mchezo wa marejeano utafanyika Azam complex , huku klabu ya Singida black stars wamepangwa kucheza na Rayon Sports kutokea nchini Rwanda ambapo wataanzia ugenini na kumalizia nyumbani nchini Tanzania.


Wadau wa soka nchini wanasema kuwa kwa upande wa Simba na Yanga hawatii shaka kusonga mbele katika hatua hiyo lakini wasi wasi unakuja kwa vilabu vya Singida na Azam kwani wamepangwa na timu ambazo kiuwezo hawapishana sana hivyo ili kuhakikisha wanafuzu hatua zinazo fuata watakiwa kuhakikisha wanafanya kazi ya ziada ili kusonga mbele kwenye mashindano hayo.


0767915473,

Lugembetimothy01@gmail.com


0/Post a Comment/Comments