Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Mchezo wa ngao ya hisani ulioashiria kufunguliwa kwa pazia la ligi kuu ya Uingereza (EPL), uliowakutanisha Crystal Palace dhidi ya Liverpool katika dimba la Wembley stadium ulitamatika kwa palace kuibuka washindi kwa mikwaju ya penalty baada ya dakika tisini kumalizika kwa sare ya 2-2.
Liverpool walipewa nafasi kubwa yakufanya vizuri katika mchezo huo lakini palace waliwashangaza wengi kwa matokeo waliyo pata, laverpool walianza kuandikisha bao mapema dakika ya dakika ya 4’ kupitia Hugo Ekitike, na baadae 17' Jean Mateta alisawazisha bao hilo kwa mkwaju wa penalty lakini Jeremie Frimpong 21’ aliongeza bao la pili na kuwafanya Liverpool kurudi kwenye uongozi , palace hawakuwa nyuma mnamo dakika ya 77’ Ismaila Sarr alisawaziha na kuufanya mchezo kuisha kwa sare ya 2-2.
Mikwaju ya penalty ndiyo iliyo amua mshindi wa mchezo huo ambapo palace waliishinda Liverpool kwa penalty 3-2, na kutawazwa kuwa mabingwa wa ngao ya hisani kwa msimu 2025-26 na wanauanza msimu kwa taji, je mwanzo huo mzuri wataushikilia mpaka kwenye michezo ya ligi kuu, majibu yatapatikana baad aya michezo kuanza rasmi agosti 15.
0767915473.
lugembetimothy@gmail.com.
Post a Comment