ARSENAL YAVUTA KITASA KUTOKA LEVERKUSEN

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports

Klabu ya Arsenal imekamilisha uhamisho wa Piero HincapiƩ akitokea Bayer Leverkusen ya Ujerumani.

Arsenal imekamilisha Dili hilo kwa €52 milioni pamoja na kipengele cha asilimia 10 ya mauzo ya baadaye, HincapiĆ© anatarajiwa kusafiri mara moja kwenda London ili kukamilisha vipimo vya afya na kusaini mkataba wa miaka mitano na The Gunners.

 HincapiĆ© ni beki mwenye nguvu na kasi pia ni mzuri one v one, mtulivu na mzoefu wa mashindano makubwa kwani msimu jana aliiwakilisha vizuri Leverkusen kwenye ligi ya mabingwa barani ulaya pamoja na timu yake ya taifa ya Ecuador kwenye mechi za kufuzu kombe la dunia na mashindano mengine.

Arsenal imekuwa ikihitaji machaguo mengi kwenye eneo la beki wa kati, hasa kutokana na majeraha ya mara kwa mara kwa wachezaji wao muhimu kama Saliba na Gabriel, hivyo HincapiƩ ni moja ya ongezo bora kutokana na ubora wake.

Kwa upande mwingine, taarifa njema zaidi ni kuwa Jakub Kiwior naye amekaribia kuondoka baada ya kukubali dili la kujiunga na Porto kwa dau la €27 milioni. Hii inaonyesha mpango kabambe wa Arsenal kusafisha na kuimarisha safu yao ya ulinzi msimu huu.

Mashabiki wa Arsenal na wadau wa soka duniani kote sasa wanaamini sasa ni wakati sahihi kwa kocha Mikel Arteta kuwapa Gunners mafanikio msimu huu kutokana na machaguo mengi na wachezaji bora waliyokuwa nao msimu huu.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments