ZINATAKIWA BILLIONI MBILI KUMG'OA FEI AZAM FC

 


Timothy Lugembe,

mwanakwetusports.

Nyota wa Azam FC, Fei Toto, bado hajatia saini mkataba mpya licha ya klabu yake kumpa ofa ya kuvutia ya kumuongeza mkataba kwa masharti mazuri zaidi.

Kwa mujibu wa taarifa, mkataba wa sasa wa Fei na Azam FC una kipengele cha “Buyout Clause” kinachosema kuwa timu yoyote inayotaka kumsajili itatakiwa kulipa dola za Kimarekani laki tano, sawa na shilingi bilioni moja na milioni mia mbili themanini na tano ili kuvunja mkataba wake wa sasa.

Klabu ya Simba SC ndiyo inatajwa kuwa na nia ya dhati ya kumsajili kiungo huyo mahiri, lakini ili hilo litekelezeke italazimika kumpa Fei kiasi hicho cha dola lakitano, ili yeye mwenyewe avunje mkataba wake na Azam.

Hadi sasa, Azam FC wamekwisha muwekea mezani ofa ya mkataba mpya ambayo wanasema ni ofa ambayo anaweza kuchukua au laa, Ofa hiyo inajumuisha mambo yafuatayo:

1. Malipo ya kusaini mkataba mpya (Sign on Fee) ya shilingi milioni mia nane .

2. Mshahara wa kila mwezi wa shilingi milioni hamsini baada ya makato ya kodi, kiasi kinachomwezesha kuingiza kipato kikubwa cha uhakika kila mwezi.

3. Ubalozi wa Azam Pesa, ambapo Fei atakuwa balozi wa chapa hiyo na kulipwa shilingi milioni 200 kila mwaka.

Licha ya ofa hiyo ya kuvutia, kiungo huyo bado hajatia saini mkataba mpya, hali inayoibua maswali mengi kuhusu hatma yake katika dirisha hili la usajili.

Kwa mujibu wa wachambuzi wa masuala ya soka, klabu inayotaka kumsajili Fei inapaswa kuwa na jumla ya fedha zinazofikia kiasi cha shilingi bilioni mbili, Hii ni baada ya kutoa shilingi bilion 1.3 kwa ajili ya kuvunja mkataba wake Azam, na kisha kumpa yeye binafsi kiasi cha shilingi milioni 800 kama malipo ya usajili (signing fee).

Swali kubwa kwa sasa linasalia kuwa, je timu zetu kongwe kutoka Kariakoo ziko tayari kutoa kiasi hicho kikubwa cha fedha kwa ajili ya kumchukua Fei? Muda utaonyesha.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments