Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Inasemekana klabu ya Yanga SC imepanga kumsajili beki wa kushoto Mohamed Hussein "Zimbwe jr " baada ya mchezaji huyo kumaliza mkataba wake na Simba na haja ongeza mkataba mpaka sasa ambapo Yanga wameonyeshwa nia ya kumsajili.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyanzo vya nadani vya klabu ya Yanga zinaeleza kuwa harakati za kumsajili beki huyo zinaweza kukamilika pindi tu atakapo tua nchini baada ya kutoka kwenye kambi ya timunya Taifa.
Taarifa kutoka ndani ya klabu ya Yanga SC zimeeleza kuwa maandalizi yote ya mkataba yamekamilika na kilichobakia ni Zimbwe Jr kuweka sahihi yake kwenye mkataba huo na kuvalishwa rasmi jezi ya kijani na njano.
Usajili wa Zimbwe Jr unatarajiwa kuimarisha kikosi cha Yanga SC kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara na mashindano ya kimataifa, Mashabiki wa Yanga wamesubiri kwa hamu ujio wa nyota huyo ambaye ameonyesha uwezo mkubwa katika mechi za za kimataifa akiwa na Simba na timu ya Taifa.
Zimbwe Jr ataongeza nguvu kwenye safu ya ulinzi ambayo tayari ina wachezaji wakongwe na chipukizi wenye vipaji, jambo linalowapa matumaini makubwa wanachama na mashabiki wa klabu hiyo kongwe nchini kuelekea michuano ya kimataifa na ligi ya ndani.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment