Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Hatua ya 16 Bora fainali ya michuano ya FIFA Club World Cup 2025 inayoendelea nchini Marekani imekamilika rasmi huku timu nane kutoka mabara matatu zikisubiri kuamua nani ataingia hatua ya nusu fainali.
Timu hizo nane ni Fluminense (Brazil), Al Hilal (Saudi Arabia), Palmeiras (Brazil), Chelsea (England), Paris Saint-Germain (France), Bayern Munich (Germany), Real Madrid (Spain), na Borussia Dortmund (Germany).
Hatua ya robo fainali inatarajiwa kufanyika siku ya Julai 4 na 5 mwaka huu ambapo Julai 4, Fluminense vs Al Hilal saa 4 :00 usiku, huku Julai 5, ndio mechi zitamalizika ambapo Palmeiras vs Chelsea saa 10:00 alfajiri, PSG vs Bayern Munich, saa 1:00 usiku, Real Madrid vs Borusia Dortmund saa 5:00 usiku, kwa saa za Africa mashariki.
Kwan mujibu wa wachambuzi wa soka ulimwenguni na takwimu wanasema kuwa timu zote zinanafasi sawa ya kufuzu nafasi ya fainali lakini anaepewa nafasi Kutwaa ubingwa huu ni PSG kutoka ufaransa kutokana na kuwa na muendelezo wa kiwango chao, je tutegemee matokeo ya kushangaza katika hatua hii baada ya hatua ya 16 bora kuwaacha watu modomo wazi?.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment