WACHEZAJI HATARINI, RATIBA KALI ZA MASHINDANO ZAIBUA WASIWASI KITAALAMU

 

Timothy Lugembe,

 Mwanakwetusports .

Ratiba ngumu ya mashindano ya mwaka 2025 imewaacha wachezaji wa soka wakiwa na uchovu, huku wataalamu wa afya na michezo wakionya kuwa ukosefu wa mapumziko ya kutosha unaweza kusababisha madhara ya muda mrefu kwa afya ya wachezaji na pia kusababisha majeruhi ya muda mrefu.

Mashindano yamekuwa yakiingiliana mwaka huu kuanzia ligi kuu za Ulaya, michuano ya bara, hadi Kombe la Dunia la vilabu lililofanyika katikati ya mwaka, Wachezaji wengi wamejikuta wakicheza kwa takribani miezi 11 mfululizo bila likizo ya maana, hali ambayo imeibua tahadhari miongoni mwa madaktari wa michezo na vyama vya wachezaji.

Kwa mujibu wa FIFPRO chama cha wachezaji wa soka duniani wachezaji wengi wamepewa wastani wa chini ya siku 20 za mapumziko kabla ya kurejea kambini kujiandaa na msimu mpya, Hii ni tofauti kubwa na miaka ya nyuma ambapo wachezaji walikuwa na zaidi ya mwezi mmoja kupumzika.

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta, hivi karibuni alilalamikia ratiba hiyo, akisema ni hatari inayosubiri kutokea na wapo kwenye hatari kubwa ya kuchoka kupita kiasi na kupata majeraha ya muda mrefu, pia Pep Guardiola baada ya kuondoshwa kwenye mashindano ya vilabu Duniani alikiri kuwa wachezaji wamechoka na anamashaka na wakavyo uanza msimu mpya , hata hivyo imeshuhudiwa Jamal Musiala mchezaji Bayer Munich akipata maheraha ya yatakayo muweka nje kwa miaez mitano.

FIFA imeshauriwa kutathmini upya kalenda ya mashindano na kuhakikisha wachezaji wanapata angalau wiki tatu za kupumzika kabla ya kuanza msimu mpya, Wadau wengi wanasema mashindano ya kimataifa, ya klabu na ligi za kitaifa yanapaswa kupangwa kwa uangalifu ili kulinda afya za wachezaji.

Wakati vilabu vikijiandaa kwa msimu mpya wa 2025/26, baadhi ya wachezaji wameanza kurejea mazoezini bila hata wiki mbili za mapumziko, hii imezua maswali mengi kuhusu uthabiti wao mwilini na kiakili kwa msimu ujao.

IgiI nyingi barani ulaya na ulimwenguni kwa ujumla zinatarajiwa kuanza mapema katikati ya mwezi Agosti mwaka huu huku wachezaji wengi wakiwa hawajapata mapumziko ya kutosha. Je, hali hii italeta matokeo gani kwa wachezaji ni jambo la kusubiri.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments