Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Mashabiki wa soka duniani wamepigwa na butwaa baada ya vigogo wawili kutoka bara la Ulaya Manchester City ya England na Inter Milan ya Italia kutupwa nje ya michuano ya Kombe la Dunia la Vilabu (FIFA Club World Cup 2025) katika hatua ya 16 bora kwa matokeo ya kushangaza.
Katika mchezo wa kusisimua uliopigwa mjini Orlando, Marekani, Manchester City walikubali kichapo cha 4-3 kutoka kwa Al Hilal ya Saudi Arabia, baada ya mechi kumalizika kwa sare ya 2-2 katika muda wa kawaida na melinya man city ilizamishwa kwenye muda wa nyongeza.
Katika mchezo mwingine uliochezwa jijini Miami, Inter Milan walitandikwa kwa mabao 2-0 na Fluminense ya Brazil, Goli la mapema dakika ya 3 kutoka kwa mshambuliaji matata Germán Cano liliwapa Wabrazil kujiamini, kabla ya Hércules kufunga la pili kwenye dakika ya 90+3 na kufunga rasmi mlango wa matumaini kwa wababe hao wa Serie A.
Kwa matokeo haya, timu zote mbili kutoka Ulaya zimeondolewa mapema kuliko matarajio ya wengi, hali inayoibua mjadala kuhusu nguvu mpya ya vilabu vya Asia na Amerika Kusini katika soka la dunia.
0767915473.
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment