TUANZEBE AISHTAKI MANCHESTER UNITED KWA UZEMBE WA KITABIBU

 


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Aliyekuwa beki wa Manchester United, Axel Tuanzebe, ameishtaki rasmi klabu hiyo kwa madai ya uzembe wa kitabibu (clinical negligence) unaohusiana na ushauri wa matibabu aliopewa wakati akiwa mchezaji wa kikosi hicho.

 beki huyo mwenye umri wa miaka 27 amepeleka kesi Mahakama Kuu, akitaka fidia kutokana na kile kinachodaiwa kuwa ni ushauri mbovu wa kiafya uliomgharimu maendeleo ya taaluma yake ya soka akiwa Old Trafford na baada ya kuondoka klabuni hapo.

Tuanzebe, ambaye aliondoka United miaka miwili iliyopita baada ya mkataba wake kumalizika, hakupata mafanikio aliyotarajiwa kutokana na msururu wa majeraha yaliyomuandama kwa miaka mingi akiwa ndani ya kikosi hicho, Wakili wake amekataa kutoa maelezo zaidi kuhusu kesi hiyo, huku klabu ya Manchester United ikitajwa kuwa tayari imewasilishiwa madai hayo.

Majeruhi ya kwanza makubwa yalitokea Oktoba 2019 alipoumia nyonga wakati wa maandalizi ya mchezo dhidi ya Liverpool, Mwezi Desemba mwaka huo, aliumia tena kwenye mchezo wa Kombe la Carabao dhidi ya Colchester United na kulazimika kumaliza msimu akiwa nje, Majeruhi ya mguu yalimsumbua pia mwanzoni mwa msimu uliofuata, na hakurejea uwanjani hadi Januari 2023 alipokuwa kwa mkopo Stoke City.

Manchester United bado haijatoa tamko rasmi kuhusu madai hayo ya mahakamani, ambayo yanakuja miaka miwili baada ya kutoa salamu za kumuaga kwa heshima kubwa kupitia tovuti yao. Ujumbe huo ulisema.

“Kuondoka kwake ni jambo la kihisia kwa mchezaji na kwa wote waliomlea ndani ya klabu kwa miaka mingi, Axel ni mtu mwenye tabia ya kipekee, na anaheshimika kwa kila mtu kama mfano bora wa mchezaji wa Manchester United.”

Kesi hii ni ya pili kwa United kuhusiana na Tuanzebe, ambapo Mwezi Novemba, iliripotiwa kwamba klabu hiyo ilipokea madai ya malipo kutoka kwa wakala aliyedai alihusika katika uhamisho wa mchezaji huyo kwa mkopo kwenda Stoke City, jambo ambalo liliripotiwa kwa Chama cha Soka (FA) kwa madai ya kuvunjwa kwa kanuni za mawakala wa soka.



0767915473.

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments